1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rais wa Korea Kusini aomba radhi kwa taifa

7 Desemba 2024

Rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini ameomba radhi kwa taifa lake kutokana na amri yake ya kutangaza sheria ya matumizi ya nguvu za kijeshi, hatua iliyozuwa ukosoaji mkubwa dhidi yake.

https://p.dw.com/p/4nrfA
Yoon Suk Yeol, Korea Kusini
Rais Yoon Suk Yeol akihutubia taifa siku ya Jumamosi (Disemba 7).Picha: Kim Soo-hyeon/REUTERS

Katika hotuba aliyoitowa muda mfupi uliopita, Rais Yoon amesema anatambuwa kuwa uamuzi wa kutangaza sheria hiyo ulisababisha mtafaruku mkubwa kwenye nchi na amewaomba raia wamsamehe.

Huku akiinamisha kichwa chake chini, Yoon amesema anakiwachia chama chake kuamua hatima yake, ikiwa aendelee au aondoke madarakani.

Soma zaidi: Kiongozi wa upinzani Korea Kusini anaonya kuhusu jaribio lingine la kutangazwa sheria ya kijeshi

Hotuba hii fupi imetolewa ikiwa ni masaa machache kabla ya bunge kujadili hoja ya kutokuwa na imani na rais huyo.

Tayari mkuu wa chama chake kinachotawala, Han Dong-hoon, amesema kwamba kujiuzulu kwa rais huyo ni jambo lisiloepukika, kwani hana tena nafasi ya kutekeleza majukumu yake kwa umma.

Upinzani unahitaji kura nane tu kati ya 108 za wabunge wa chama tawala kuweza kumuondosha Yoon madarakani.