Rais wa Somalia aongoza vikosi kupambana na al-Shabaab
19 Oktoba 2023Taarifa ya ofisi ya rais huyo siku ya Jumatano (Oktoba 18) ilisema Mohamud anapanga kuanzisha awamu ya pili ya operesheni dhidi ya kundi hilo la wapiganaji katika majimbo ya kusini magharibi na eneo la Juba.
Mnamo Oktoba 7, kiongozi wa jimbo la kusini magharibi, Abdiaziz Hassan Mohamed, na maafisa wakuu wa usalama walifanya mkutano na kutangaza kuanza kwa operesheni dhidi ya al-Shabaab.
Soma zaidi:Kenya kuitangazia vita al-Shabaab
Marekani yatowa dola $5M kumpata kiongozi wa al-Shabaab
Katika kipindi cha miezi michache iliyopita, rais wa Somalia alikuwa katika mikoa ya kati ambako bado serikali haijafanikiwa kurejesha udhibiti wa miji mikubwa kutoka kwa washirika hao wa kundi la al-Qaida, licha ya kuungwa mkono na wanamgambo wa koo katika mashambulizi hayo.