SiasaAsia
Rais Yoon wa Korea Kusini aomba radhi kwa raia wake
7 Desemba 2024Matangazo
Rais wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol ameomba radhi kwa taifa lake kutokana na amri aliyotangaza ya sheria ya kijeshi mapema wiki hii, hatua hiyo ilizua ukosoaji mkubwa dhidi yake.
Katika hotuba yake ya leo, Rais Yoon amesema anatambua kuwa uamuzi wa wake wa kutangaza sheria hiyo ya kijeshi ulisababisha sintofahamu kubwa kwenye nchi na amesema anakiachia chama chake kuamua hatima yake, ikiwa aendelee au aondoke madarakani.
Soma zaidi.Rais wa Korea Kusini aomba radhi kwa taifa
Hotuba hii fupi imetolewa ikiwa ni masaa machache kabla ya bunge la nchi hiyo kuanza kujadili hoja ya kumwondoa madarakani rais huyo. Kiongozi wa chama chake amesema Rais Yoon Suk Yeol hawezi kukwepa kuondoka madarakani.