Rutte kuanza uongozi wa NATO
30 Septemba 2024Matangazo
Katibu Mkuu anayemaliza muda wake, Jens Stoltenberg, ameliambia shirika la Habari la Reuters katika mahojiano siku ya Jumatatu (Septemba 30) kwamba nchi wanachama wa NATO hazipaswi kujizuia kutoa msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine na kutokana na vitisho vya Rais Vladimir Putin wa Urusi anayesema anaweza kutumia silaha za nyuklia.
Soma zaidi: Putin asema Urusi itatimiza malengo yote yaliyowekwa Ukraine
Stoltenberg, atakabidhi uongozi wa Jumuiya ya NATO kwa Rutte baada ya kuhudumu kwa muongo mmoja.