1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Takbrini watu 300 wafariki kwa Kimbunga Yagi

20 Septemba 2024

Idadi ya waliofariki kutokana na Kimbunga Yagi nchini Myanmar imefikia watu 293, huku wengine 89 wakiwa haijulikani walipo.

https://p.dw.com/p/4ktQo
Mafuriko makubwa kutokana na Kimbunga Yagi yameangamiza maisha ya watu zaidi ya 600 kusini mashariki mwa Asia.
Mafuriko makubwa kutokana na Kimbunga Yagi yameangamiza maisha ya watu zaidi ya 600 kusini mashariki mwa Asia.Picha: Sai Aung Main/AFP/Getty Images

Hayo yameelezwa na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ya kusini mwa Asia, huku vyombo vya habari vikiripoti kuwa msaada wa kwanza wa kigeni umeanza kuwasili nchini humo.

Zaidi ya ekari 660,000 za mpunga na mazao mengine ziliharibiwa na mafuriko huku wanyama zaidi ya 100,000 wakifariki.

Soma zaidi: Idadi ya waliokufa kwa kimbunga yafikia watu 200

Kimbunga Yagi kiliyapiga maeneo ya kaskazini mwa mataifa ya Vietnam, Laos, Thailand na Myanmar zaidi ya wiki moja iliyopita.

Mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi kutokana na mvua hiyo yamesababisha vifo vya watu 613 katika eneo hilo.