Tanzania yakosolewa oparesheni komesha ukahaba
6 Novemba 2023Operesheni hiyo inafanywa katika kile kinachoelezwa ni kulinda utamaduni wa kitanzania kwa kukabiliana na vitendo vinavyoenda kinyume na maadili. George Njogopa na taarifa zaidi.
Wengi wanaikosoa operesheni hiyo wanasema inaendeshwa kwa njia ya udhalilishaji kwani wahusika wake wanaletwa kwenye kamera na sura zao kuonyeshwa hadharani.
Baadhi ya nyumba ambazo zinadaiwa kuwa sehemu za madanguru huvamiwa na maafisa wa serikali huku wale wanakutwa wakimulikwa na kamera za wazi na picha zao kuwekwa hadharani.
Soma pia:Pakistan yawakamata watu 10 kwa kuuza binadamu
Ingawa baadhi wanasema hatua ya serikali kukabiliana na ukahaba ni jambo linaloonekana kuwa jema machoni kwa wengi, hata hivyo wanakosoa kutokana na jinsi linavyotweza utu wa wale wanaohusika.
Mwanaharakati Samsoni Mbunila anawatupia lawama maafisa wanaendesha operesheni hiyo akisemahaijalenga kuleta ufumbuzi wa kudumu katika kukabiliana na tatizo hilo.
Wachambuzi: Serikali itafute mwarobaini wa tatizo
Kumekuwa na maoni mengi mchanganyiko tangu kutangazwa kunzishwa kwa opereshini hiyo ambayo haijaelezwa kama itakuwa ya kudumu au la.
Baadhi wanaona mamlaka za dola zinapaswa kusaka mwarubaini kwa kudumu kuhusiana na madangurioi yanadaiwa kuwepo katika maeneo ya mijini.
Lakini hata hivyo, baadhi ya makundi ya vijana wanadaiwa kuwa karibu na maenero hayo wamekuwa wakishutumu hatua ya serikali kuyavamia maemeo hayo.
Soma pia:Polisi ya kimataifa yamkamata mfanyabiashara haramu ya binaadamu
Katika moja ya operesheni zake, mkuu wa wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule aliwagiza kina dada wote walionaswa kwenye msako huo kwenda kijisalimisha katika vituo vya polisi kwa ajili ya kuhojiwa.
Serikali inasema uendeshaji wa vikundi vya kikahaba ni kinyume cha sheria ingawa wengi wanaotumbukia katika biashara hiyo wanasukumwa na ukali wa maisha.