1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume ya uchaguzi Kenya yapendekeza mabadiliko.

Thelma Mwadzaya17 Machi 2022

Maandalizi ya uchaguzi mkuu yameshika kasi nchini Kenya.Tume ya uchaguzi na mipaka,IEBC,inalisukuma bunge la taifa kuyapa uzito matokeo yaliyochapishwa na nakala za maafisa wake kabla ya kutangaza matokeo ya urais.

https://p.dw.com/p/48dzg
Kenia Symbolbild Wahlen und Social Media
Picha: AFP/T. Karumba

Wakati huohuo, kiongozi wa ODM Raila Odinga aliye ziarani mjini London amemtetea Rais Uhuru Kenyatta kwa juhudi zake za kupambana na ufisadi. Naibu wa rais William Ruto naye anashikilia kuwa madeni ya nje yanawazonga wakenya.

Akizungumza kwa mara ya kwanza muda mfupi baada ya kupata ridhaa rasmi ya kuwa afisa mkuu mtendaji wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC, Marjan Hussein Marjan aliweka bayana kuwa ipo haja ya kuwa na mfumo wa pili wa kuaminika kuwawezesha kufanya uchaguzi wa huru na haki.

Soma zaidi:Ruto kugombea urais wa Kenya kwa tiketi ya UDA

Alisema hata kabla ya mabadiliko ya sheria mahakama ya juu ilishasisitiza kuwa matokeo rasmi ni yale ambayo yapo kwenye fomu rasmi "maafisa watatakiwa kuzifikasha kwenye eneo la kujumuisha matokeo ya uchaguzi" Alisema Marjani katika mahojiano hayo.

IEBC:Yapendekezo matokeo yaliochapwa kwa karatasi

Tume ya IEBC inapendekeza mageuzi mazito yanayoegemea matokeo yaliyochapishwa kwenye makaratasi badala ya kieletroniki endapo mushkil utazuka.Kimsingi,afisa mratatibu huenda akalazimika kukifikia kituo cha kuhesabu kura cha eneo bunge husika.

Emdapo sintofahamu inatokea kati ya matokeo ya elektroniki na yaliyochapishwa kwenye makaratasi basi nakala ya maafisa wa uchaguzi wa IEBC ndiyo itakayokuwa msema kweli.

Kenia Wahl 2013
wakala wa uchaguzi KenyaPicha: picture alliance/dpa/K. Dhanji

Kwenye pendekezo jengine,kikosi cha IEBC kinashauri maafisa wake waruhusiwe kuzunguka nje ya vituo vya kupigia kura kusaka mawasiliano mujarab ili waweze kuwasilisha matokeo kielektroniki.

Soma zaidi:Odinga aidhinishwa rasmi na Azimio la Umoja kugombea urais

Kwa sasa sheria inawabana maafisa hao kutuma matokeo kielektroniki nje ya maeneo yaliyoteuliwa.Itakumbukwa kuwa mwaka 2017 tume ya IEBC ilishindwa kuwasilisha matokeo kutokea vituo alfu 10 ambavyo havikuwa na mtandao wa 3G wa mawasiliano.

Kadhalika IEBC inataka kipengee kinachoipa ridhaa mahakama ya juu kufutilia mbali uchaguzi wa rais wanaposhindwa kuwasilisha matokeo kieletroniki kutokuwa na makali.Kadhalika, IEBC inapendekeza kuruhusiwa kuwathibitisha wapiga kura kielektroniki na pia kuwaona.

Kimsingi,maafisa wake wapate ridhaa kuandika maelezo ya wapiga kura pale mashine za kielektroniki za mfumo wa KIEMS zinapofeli.

Mapendekezo ya IEBC yazua wasiwasi wa wizi wa kura

Mapendekezo hayo yamezua wasiwasi kuwa huenda yakaufungua mwanya wa kuhitilafianana matokeo ya uchaguzi, jambo ambalo ameliangazia  naibu wa rais William Ruto anayewania uongozi wa taifa kupitia chama cha UDA kilicho mshirika mkuu wa muungano wa Kenya Kwanza.

Kenia Nairobi Demonstration Odinga Anhänger
Wakereketwa wa siasa KenyaPicha: Getty Images/AFP/T. Karumba

Akiwa London wiki iliyopita William Ruto aliliangazia hilona hii leo anasisitiza kuwa hali ya wakenya kiuchumi ni mbaya na madeni ya nje yanawazonga, huku viongozi waliopo wakibadili katiba ili kugawana vyeo.

"Wale handshake brothers hawajui umasikini ni nini" Alisema Ruto huku akishangiliwa na wafuasi wake waliojitokeza katika mkutano huo wa kunadi sera zake.

Soma zaidi:Ruto aitaka tume ya IEBC kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru

Kauli hizo zinaungwa mkono na Musalia Mudavadi wa ANC, chama ambacho ni chama mwenza cha muungano wa Kenya Kwanza.

Kwa upande wa pili chama cha Jubilee kimemtimua Seneta wa Kiambu Kimani wa Matangi aliyekuwa kiranja wa chama tawala kwenye baraza la Senate.Hii ni baada ya kujiunga na chama cha UDA cha naibu wa Rais William Ruto.

Wanaomuunga mkono Rais Uhuru wanamshinikiza naibu wa rais kujiuzulu.Masom Leshoomo ni mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Samburu.

Odinga amkingia kifua Uhuru dhidi ya hoja za Ruto

Kiongozi wa Orange Democratic Movement, ODM, Raila Odinga amemtetea rais Uhuru Kenyatta anayepambana na jinamizi la ufisadi serikalini.Kwa mtazamo wake kiongozi wa taifa anakabiliana na vikwazo kutoka kwa naibu wa rais na wapambe wake.

Kenia Building Bridges Initiative (BBI)
Raila Odinga mgombea Urais Kenya kupitia ODMPicha: AFP/T. Karumba

Raila Odinga yuko kwenye ziara ya siku 5 nchini Uingereza alikopata nafasi kuhutubia kikao muhimu cha Chatham House na pia kukutana na wakenya.

Amesindikizwa na Gavana wa Kitui Charity Ngilu, wa Mombasa Ali Hassan Joho, mbunge wa Suna Mashariki na katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyakazi, COTU, Francis Atwoli.