Tusk: Nitapambana kuisadia Ukraine dhidi ya Urusi
12 Desemba 2023Matangazo
Katika taarifa yake bungeni wakati alipoliwasilisha baraza lake la mawaziri, amesema hatowasikiliza wanasiasa wa Magharibi waliochoshwa na suala la Ukraine.
"Nataka kusema kwamba ni jukumu la Poland, jukumu la serikali mpya, na pia ni jukumu letu sote kusema kwa sauti na uwazi kabisa kwamba jumuiya yote ya Mataifa ya Magharibi inaonyesha kujitolea kuisaidia Ukraine katika vita hivi. hicho ndicho nitakachokifanya kuanzia siku yangu ya kwanza kama Waziri Mkuu" Alisema Tusk
Soma pia:Tusk aahidi kuendelea kuisaidia Ukraine
Poland imekuwa muungaji mkono mkubwa kijeshi na kisiasa wa Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi Februari mwaka jana. Tusk ambaye ni rais wa zamani wa Baraza la Ulaya aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Poland jana Jumatatu.