1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yafunga ubalozi Niger kufuatia mapinduzi

3 Januari 2024

Ufaransa imeufunga ubalozi wake Niger hadi itakapotoa taarifa nyingne, ikisema kazi ya wafanyakazi wake wa kidiplomasia imekuwa ngumu tangu mapinduzi ya kijeshi katika taifa hilo la Afrika Magharibi ya miezi 5 iliyopita

https://p.dw.com/p/4aoOM
Niger Französische Botschaft in Niamey
Maandamano nje ya ubalizi wa Ufaransa mjini Niamey Julai 30.2023Picha: AFP

Wizara ya Mambo ya Nje ya ufaransa imesema ubalozi umezuiwa shughuli zake, wafanyakazi wamewekewa vizuizi na wanadiplomasia wamezuiwa kusafiri kwenda Niger.Aidha imeongeza kwa kusema ubalozi unaendelea na kazi zake kutoka Paris na shughuli za kibalozi zinaendelea kutekelezwa na ubalozi mdogo wa Ufaransa katika kanda hiyo. Niger, yenye wakazi karibu milioni 26, ilikua mshirika wa kidemokrasia wa Marekani,Ufaransana nchi nyingine za Ulaya katika mapambano dhidi ya makundi ya wenye itikadi kali katika eneo la Sahel, ambapo makundi haya kwa sasa yanaelezwa kupata nguvu.