1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uholanzi yataka kujiondoa mpango wa uhamiaji wa Ulaya

18 Septemba 2024

Serikali ya siasa kali za mrengo wa kulia nchini Uholanzi, imesema imeiomba Umoja wa Ulaya kujiondoa katika kanuni za uhamiaji za umoja huo, ili iweze kudhibiti ujio wa wahamiaji wapya.

https://p.dw.com/p/4kkuF
Uholanzi The Hague 2024 | Geert Wilders kwenye mjadala wa bungeni
Mwanasiasa mwenye itikadi kali Geert Wilders ana usemi mkubwa kwenye serikali mpya ya Uholanzi.Picha: John Beckmann/Orange Pictures/BEAUTIFUL SPORTS/picture alliance

Waziri wa Uhamiaji Marjolein Faber amesema katika mtandao wa X kwamba ameiarifu Halmashauri Kuu ya Umoja huo kwamba anataka nchi hiyo ijiondoe katika kanuni hizo za EU ili waweze kusimamia wenyewe sera zao za juu ya waomba hifadhi. 

Serikali hiyo iliyo madarakani tangu mwezi Julai inayoongozwa na Geert Wilders inapanga kutangaza mgogoro wa kitaifa wa waomba hifadhi hali itakayoipa nafasi ya kudhibiti mipaka yake bila idhini ya bunge. 

Hata hivyo, Umoja huo unatarajiwa kupinga nia hiyo ya Uholanzi kwa kuzingatia kuwa nchi wanachama wa Umoja huo ziliridhia makubaliano ya pamoja ya uhamiaji yaliyofikiwa mwezi Desemba mwaka 2023.