1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yaashiria kuhusika na mauaji ya Kirillov

17 Desemba 2024

Idara ya usalama wa taifa ya Ukraine, SBU, imeashiria kwamba imehusika na mauaji ya kamanda wa kitengo cha kemikali na kibaolojia cha wanajeshi wa Urusi, Jenerali Igor Kirillov, mapema leo Jumanne.

https://p.dw.com/p/4oG1F
Russland | Ort der Explosion bei der  Igor Kirillow, und sein Assistent getötet wurden
Muonekano wa eneo la mlipuko, ambao uliua kamanda wa askari wa ulinzi wa kemikali, kibaolojia na mionzi ya jeshi la Urusi, Igor Kirillov, na msaidizi wake, Urusi, Picha: ALEXANDER NEMENOV/AFP via Getty Images

Shirika la habari la Urusi, Interfax, na mashirika mengine ya habari yamezinukuu duru ndani ya SBU zikithibitisha kuhusika na mauaji ya jenerali huyo. Duru hizo za SBU zimesema Jenerali Kirillov alikuwa muhalifu na amekuwa akilengwa kwa madai ya kuamuru matumizi ya silaha za kemikali dhidi ya wanajeshi wa Ukraine katika uwanja wa mapambano. Uingereza na Marekani ziliwahi kuishutumu Urusi kutumia sumu aina ya chloropicrin dhidi ya wanajeshi wa Ukraine kinyume na Mkataba wa Silaha za Kemikali. Urusi imekanusha tuhuma hizo na kusema haimiliki tena aina hiyo ya silaha za kemikali.