JamiiHaiti
UN: Zaidi ya watu 530 wauawa ndani ya mwaka huu nchini Haiti
21 Machi 2023Matangazo
Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na haki za binadamu imesema ina wasiwasi kwamba machafuko mabaya yanaongezeka na kushindwa kudhibitiwa.
Msemaji wa ofisi hiyo Marta Hurtado amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva,Uswisi kwamba mpaka kufikia tarehe 15 mwezi huu wa Machi watu 531 wameshauwawa na 300 wamejeruhiwa wakati 277 wakitekwa nyara katika matukio yaliyohusisha magenge hayo.
Soma pia: Guterres aomba kikosi cha kimataifa kipelekwe Haiti kuzima uhalifu
Visa hivyo vimefanyika zaidi katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince.