1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUrusi

UN: Tuna wasiwasi na sera ya Urusi kutoa uraia kwa waukreine

Hawa Bihoga
9 Oktoba 2023

Umoja wa Mataifa umeonesha wasiwasi wake mkubwa juu ya watu "kukabidhiwa kwa wingi" pasi za kusafiria za Urusi, katika eneo la Ukraine ambalo linadhibitiwa na Moscow na wale wanaozikataa wakinyimwa huduma muhimu.

https://p.dw.com/p/4XJ4l
Symbolbild I UN - Mehrheit verurteilt Annexionen Moskaus
Umoja wa Mataifa ukiwa katika vikao vyake vya kawaidaPicha: Cia Pak/UN Photo/ Xinhua/picture alliance

Ofisi ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) ilisema wakaazi ambao hawachukuwi uraia wa Urusiwananyimwa huduma muhimu za umma na wako katika hatari kubwa ya kuzuiliwa kiholela.

Naibu mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Nada Al-Nashif, alisema katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu baada ya Urusi kufanya shambulio kamili la silaha dhidi ya Ukraine, kumeshuhudiwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu.

"Tunaendelea kushuhudia ukiukwaji wa wazi na usio na kikomo wa haki za binadamu," alisema Al-Nashif.

Soma pia:UN: Urusi inatumia mateso ya kikatili nchini Ukraine

Nada aliliambia Baraza la Haki za Kibinadamu katika mjadala kuhusu ripoti ya hivi karibuni ya OHCHR kuhusu haki nchini Ukraine kwamba wamekuwa na wasiwasi mkubwa wa sera inayotekelezwa katika eneolinalodhibitiwa na Urusiya kuwapa wakaazi uraia wa Urusi.

Alisema watu ambao hatokubali pasipoti za Urusi wanatengwa, kunyimwa huduma muhimu za kijamii kama vile usalama na afya

"Hii pia huongeza hatari ya kuwekwa kizuizini kiholela kwa wale wanaokataa." Alisisitiza katika uchangiaji wake.

Kwanini Urusi inalazimisha kutoa uraia?

Urusi kwa miaka mingi imekuwa ikitoa hati za kusafiria kwa raia wa Ukraine katika maeneo ya mashariki ya Donbas yanayoshikiliwa na watu wanaotaka kujitenga wanaoiunga mkono serikali ya Moscow na pia katika eneo lililokaliwa la Crimea.

Tangu Rais Vladimir Putin aanzishe uvamizi wake kamili kwa Ukrainemnamo Februari 2022, sera ya utolewaji wa hati imekuwa ikizingatiwa zaidi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Mikhail Metzel/POOL/TASS/dpa/picture alliance

Msururu wa mahitaji ya kawaida, kama vile kupokea marupurupu ya serikali, kutafuta kazi na kupata matibabu kunahitaji nyaraka zilizotolewa na Urusi.

Soma pia:Umoja wa Mataifa wasema haki za binaadamu zimedorora Urusi

Putin alitia saini amri mnamo Aprili ambayo inaruhusu raia wa Ukrainia katika maeneo yanayokaliwa na uwezekano wa kufukuzwa ikiwa hawatapata hati ya kusafiria ya Urusi kufikia Julai 1, 2024.

Naibu kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa alisema mzozo wa Ukraine unaendelea kuporomosha misingi ya utu na ubinadamu.

"Mateso yamesalia kuwa ni ukweli wa kutisha kwa raia na wafungwa wa vita wanaoshikiliwa na Urusi."

Waathirika "wanaelezea ukatili ambao ni vigumu kuufikiria", ikiwa ni pamoja na shoti za umeme, unyanyasaji wa kijinsia na vipigo vikali, aliongeza.

 "Wafungwa wengi pia walilazimishwa kuisifu Urusi, kujifunza na kuimba nyimbo za Kirusi na wakapata vipigo vikali kwa kushindwa, au kuzungumza Kiukreni," Nashif aliliambia Baraza hilo la Umoja wa mataifa.

Aliongeza kwamba Moscow haijafanya lolote ikiwemo kuwajibisha vikosi vyake dhidi ya uvunjiofu wa haki za binadamu na b adala yake sheria mpya inatoa msamaha kwa wafanyakazi wa Urusi waliokabiliwa na shutuma za uhalifu.

UN: Hakuna dalili za kuwarudisha watoto wa Ukraine

Katika muendelezo wa mjadala huo Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR ilisema kuwa ina "wasiwasi mkubwa" kwamba hakuna mfumo uliowekwa wa kuwarudisha watoto wa Ukreine waliohamishiwa Urusi au eneo lingine linalodhibitiwa na Urusi.

Watoto nchini Ukraine wahofia kifo

Soma pia:UN: Vita vya Ukraine vimesababisha ukiukwaji wa haki

Mwakilishi wa Moscow Yaroslav Eremin aliliambia Baraza la Haki za Kibinadamu kwamba OHCHR imeendelea kusafisha uhalifu unaofanywana mamlaka ya Kyiv na kuhamisha lawama kwa Urusi.

"Kimsingi hatukubaliani mbinu, maudhui na hitimisho la ripoti ya OHCHR." Alisema