UNICEF yasaka dola bilioni 9.9 kwa watoto maeneo ya vita
5 Desemba 2024Matangazo
Mkurugenzi mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell, amesema kwenye taarifa yake ya leo kwamba kiwango cha watoto wanaoteseka na wenye mahitaji kimefikia hali ambayo haijawahi kutokea kwenye historia ya ulimwengu, na kwamba wengine wengi wanaendelea kuathirika kila siku.
Fedha hizo zitaelekezwa kwa watoto milioni 109 na kusaidia kwenye miundombinu ya kimsingi ya afya, huduma za afya ya akili, maji na elimu, lishe na mapambano dhidi ya dhuluma za kijinsia.
Soma zaidi: UNICEF: Mamilioni ya wasichana wadhalilishwa kingono
Sehemu kubwa ya fedha hizo ni kwa ajili ya Afghanistan, Sudan, Kongo, Palestina na Lebanon.
Kampeni hii ya UNICEF inatangazwa wakati operesheni za misaada ya kibinaadamu zikikumbwa na uhaba mkubwa wa fedha kote ulimwenguni.