1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Urusi yadai kuzima mashambulizi ya Ukraine katika ardhi yake

30 Desemba 2023

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema imedungua ndege 32 zisizo na rubani zilizotumwa na Ukraine kuishambulia miji yake.

https://p.dw.com/p/4aizj
Ukraine Krieg | Russische Raketen in Charkiw
Maroketi yakirushwa kutoka Belgorod kuelekea Ukraine: 09.03.2023Picha: Vadim Belikov/AP Photo/picture alliance

 Hayo yanajiri siku moja baada ya mashambulizi makubwa ya Urusi katika miji mbambalimbali ya Ukraine yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 30 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 150.

Maafisa wa wizara hiyo wamesema mikoa iliyokuwa imelengwa ni ile ya magharibi ya Bryansk, Oryol na Kursk karibu na mpaka na Ukraine pamoja na mji mkuu Moscow. Urusi imedai pia kuahiribu maroketi 13 katika mkoa wa kusini wa Belgorod ambako mtu mmoja ameuawa na wanne kujeruhiwa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  limekutana hapo jana kujadili hali nchini Ukraine, baada ya nchi hiyo na washirika wake wa Magharibi kuomba mkutano wa dharura kujadili mashambulizi makubwa yaliyoendeshwa na Urusi.

Baada ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na wanachama wa baraza hilo ambao ni Marekani, Ufaransa na Uingereza, wamelaani mashambulizi hayo.