1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Urusi yapambana na wanajeshi wa Ukraine waliovuka mpaka

7 Agosti 2024

Majeshi ya Urusi yanapambana na vikosi vya Ukraine vilivyouvamia mji wa mpakani wa Kursk uliopo magharibi mwa Urusi.

https://p.dw.com/p/4jDL5
Urusi | Mkoa wa Kursk
Athari za mapambano yanayoendelea.Picha: Acting Governor of Kursk Region Alexei Smirnov/Telegram/REUTERS

Gavana wa eneo hilo Alexei Smirnov, amesema maelfu ya raia wameondolewa kutokana na mapigano na hali imedhibitiwa.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema vikosi vya Ukraine vilijipenyeza kuanzia jana na hivyo ilitumia ndege na mizinga kuvikabili vikosi hivyo.

Urusi imesema operesheni ya kuvikabili vikosi hivyo inaendelea. Ukraine kwa upande wake haijasema chochote juu ya kuhusika na tukio hilo.