1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi 130 wa dunia kujadili Gaza, Ukraine na Sudan

19 Septemba 2024

Zaidi ya viongozi 130 wa dunia watakutana wiki ijayo katika makao mkuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York marekani, kujadili kuhusu masuala mbalimbali ya migogoro ya kibinaadamu.

https://p.dw.com/p/4kpHN
Marekani New York | Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linamsikiliza mwakilishi wa WHO Dkt. Mike Ryan kuhusu hali ya Mashariki ya Kati
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linamsikiliza mwakilishi wa WHO Dkt. Mike Ryan kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, New York.Picha: Michael M. Santiago/AFP/Getty Images

Viongozi hao wataangazia pia masuala ya hali ya hewa pamoja na vita vya Mashariki ya Kati na Ulaya vinavyotishia kutanuka kutokana na kasi ndogo ya juhudi za kuimaliza migogoro hiyo. Vita vya Gaza, Ukraine na Sudan vitakuwa ndio mgogoro mikuu mitatu itakayopewa kipaumbele katika mkutano huo huku wanadiplomasia na wachambuziwakisema hawatarajii maendeleo yoyote kuelekea amani. Mkutano wa kila mwaka wa viongozi wa dunia huashiria kufunguliwa kwa kikao cha kila mwaka cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na mara nyingi huwa fursa ya kufanyika mikutano ya kidiplomasia.