1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wadau:Tunataka mgombea mwenza mwanamke Kenya

Musa Naviye13 Mei 2022

Joto la uchaguzi mkuu nchini kenya likizidi kupanda, shinikizo la wadau wa masuala ya wanawake nchini humo wamtaka mgombea urais kupitia chama cha Azimio la Umoja Raila Odinga, kuchagua mgomea mwenza mwanamke.

https://p.dw.com/p/4BFkh
Kenia Symbolbild Wahlen und Social Media
Picha: AFP/T. Karumba

Uchaguzi mkuu huo, utakaohusisha kuchaguliwa kwa rais wa 5 wa Kenya atakayetwaa uongozi kutoka kwa rais wa sasa anayeondoka Uhuru Kenyatta ukikaribia, mirnimo ya kisiasa inazidi kushika kasi huku, wadhifa wa naibu rais umeibua shinikizo huku makundi na viongozi wa kike wakihimiza wadhifa huo wa mgombea mwenza kupewa mwanamke.

Shirika la Maendeleo ya Wanawake limetoa shinikizo kwa kinara wamuungano wa kisiasa wa Azimio la Umoja wa One Kenya, Raila Odinga, kumchagua mgombea mwenza wa kike kujaza wadhifa huo.

Soma zaidi:Changamoto za kiusalama kuhusu uchaguzi Kenya

Kupitia mwenyekiti wa muungano huo, Rehab Muiu anasema wakati umefika kwa wanawake kupewa nafasi za juu za uongozi ikizingatiwa hatua iliyopigwa na mwanamke nchini Kenya.

"Tunaomba kwa unyenyekevu hii kiti ya pili tupewe kwakweli” Alisisitiza huku akionesha kwamba wanawake kwa sasa wanao utayari wa kushika mamalaka hayo ya juu nchini.

Wagombea: wanawake jitokezeni mkapige kura

 Wakizungumza wakiwa jimbo la Kisumu, kinara chama cha Narc Kenya Martha Karua ambaye ni mmoja wa watu 10 waliojitokeza kupigwa msasa kwa wadhifa wa mgombea mwenza alisisitiza, wapiga kura kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura wanawake ili kutwaa nyadhifa za kisiasa.

Aidha amewataka wanasiasa wanawake kutokata tamaa katika kipindi hiki ambacho kunashuhudiwa vikumbo vya kisiasa kuwania nyadhifa za uwakilishi.

"Mambo ya siasa watu uahidiwa, kila mtu akisimama anaambiwa ni wewe" Aliwaambia wanasiasa wanawake na kuwataka kutokata tamaa pale ambapo hawatapita katika kinya'anyiro hicho cha kidemocrasia.#

Soma zaidi:Kenya: Wadau wasisitiza amani katika uchaguzi Kisumu

Naye mwakilishi wa kike jimbo laMuranga Sabina Chege, ambaye pia alipigwamsasa katika wadhifa wa mgombea mwenza katika muungano wa azimio la umoja wa One Kenya ameunga mkono swala la wanawake kuchaguliwa katika nyadhifa za kisiasa kauli anayosema itasaidia mabunge  nchini kuzingatia thuluthi 2 ya usawa wa kijinsia huku akiahidi kushirikiana na Odinga kwenye wadhifa wa urais.

Nchini Kenya, takriban wanawake 173 kati ya idadi jumla ya viongozi 1,883 waliochaguliwa ndio wanashikilia nyadhifa za kupigiwa kura, hii ikiwa ni kulingana na ripoti ya mwaka 2018 iliyoandaliwa na shirika la National Democratic Institute – NDI kwa ushirikiano na muungano wa wanawake wanasheria FIDA Kenya, hata hivyo ni iai iliyoongezeka kutoka 145 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Maafisa wa serikali ya Kenya wanaowania viti vya kisiasa wajiuzulu