Waziri Mkuu wa zamani wa India Manmohan Singh afariki dunia
27 Desemba 2024Waziri Mkuu wa zamani wa India, Manmohan Singh, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.
Singh, anayekumbukwa kama mbunifu wa mageuzi ya kiuchumi na mkataba wa kihistoria wa nyuklia na Marekani, aliaga dunia baada ya kuugua magonjwa yanayohusiana na uzee.
Mchumi mashuhuri aliyehitimu Cambridge na Oxford, Singh aliiongoza India kwa miaka 10 kuanzia 2004, na alileta mageuzi makubwa ya kiuchumi alipokuwa waziri wa wa fedha mwaka 1991.
Soma pia:Waziri mkuu wa India ziarani Afrika
Hata hivyo, muhula wake wa pili ulitawaliwa na kashfa za ufisadi zilizochangia kushindwa kwa chama chake cha Congress, mnamo 2014.
Singh alijitahidi kuimarisha uhusiano wa India na majirani zake, na alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza mwenye asili ya Singa Singa. Anakumbukwa na viongozi wa ndani na kimataifa kwa mchango wake mkubwa kwa taifa na diplomasia ya kimataifa.