Yemen yapoteza mawasiliano ya intaneti baada ya shambulio
21 Januari 2022Kulingana na shirika la utetezi wa haki la Netblocks, usumbufu ulianza majira ya saa moja asubuhi na kuliathiri shirika la mawasiliano linalomilikiwa na serikali la TeleYemen ambalo linahodhi upatikanaji wa mtandao kwa nchini humo. TeleYemen sasa linaendeshwa na waasi wa Houthi ambao wameushikilia mji mkuu wa Yemen Sanaa tangu mwishoni mwa mwaka 2014.
Kituo cha San Diego cha Uchambuzi wa Data ya Mtandao kiIicho chini ya kampuni ya mtandao ya CloudFlare yenye makao yake mjini San Francisco pia kilithbainisha kukatika kwa mtandao wa Intanet kwa nchi nzima kulianza wakati huo wa asubuhi. Zaidi ya saa 12 baadae kasi ya intanet imesalia kuwa chini.
Soma pia: Wahouthi kuwaondoa wanajeshi kutoka bandari za Yemen
Kituo cha habari cha satelaiti kinachomilikiwa na waasi wa Houthi cha Al-Masirah, kilisema kwamba mashambulizi yalianza kwenye jengo la mawasiliano ambapo watu waliuwawa na wengine kujeruhiwa vibaya.
Kituo hicho kulitoa picha za watu wakichimbua kifusi kutafuta miili ya waliouwawa huku milio ya risasi ikisikika. Wafanyakazi wa msaada ya dharura waliwasaidia manusura waliokuwa na majeraha yaliovuja damu.
Wakati huo huo Al-Masirah kimezungumzia shambulio lingine la anga leo ( Ijumaa ) kwenye jela mkoani Saada Kaskazini mwa Yemen ambako nako watu waliuwawa na wengine kujiruhiwa vibaya. Hakukuwa na uthibitisho wa moja kwa moja idadi ya watu waliojeruhiwa kwenye mashambulio hayo.
Muungano unaoongozwa na Saud Arabia unaopambana na waasi wa Houth ulikiri kufanya mashambulio ya anga ili kuharibu uwezo wa wanamgambo waliokuwepo karibu na bandari ya Hodeida, alioiita kitovu cha uharamia na ulanguzi wa silaha za Iran nyuma ya waasi wa Houthi.
Kebo ya internet chini ya bahari yashambuliwa
Kebo ya chini ya bahari ya FALCON hubeba intaneti hadi Yemen kupitia Bandari ya Hodeida kando ya Bahari Nyekundu kwa kwa ajili ya shirika la mawasiliano laTeleYemen.Kebo zingine za FALCON zinatua katika bandari ya mashariki ya mbali ya Yemen ya Ghaydah pia, lakini idadi kubwa ya wakazi wa Yemen wanaishi magharibi yake kando ya bahari nyekundu.
Soma pia: Mapigano Yemen yatishia mpango wa amani Hodeidah
Hapo awali TeleYemen ilisema,hii ni mara ya pili kukatika kwa mawasiliano ya intaneti nchini Yemen, awali ilikuwa mwaka 2020 ambapo ilisababishwa na nanga ya meli hatua iliotatiza mtandao kwa nchi nzima.
Nyaya za ardhini kwenda Saudia Arabia zimekatwa tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen, wakati miunganisho wa nyaya zingine mbili za chini ya bahari bado hazijafanywa katikati ya mzozo. Iliongeza TeleYemen.
Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia uliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2015 ili kuunga mkono vita hivyo ambavyo vimegeuka kuwa vibaya zaidi ulimwenguni, na kukabiliwa na ukosoaji wa kimataifa juu ya mashambulizi ya anga yanayouwa raia na kulenga miundombinu ya nchi. Huku waasi wa Houthi wakitumia askari watoto na kufukia mabomu ardhi nchini kote.
Mashirika ya kiutu yaingilia kati.
shirika la Madaktari wasio na mipaka( MDS ) katika taarifa tofauti waliweka idadi ya watu waliojeruhiwa pekee ambao ni takriban 200.
Ahmed Maat mkuu wa ujumbe wa shirika hilo nchini Yemen amenukuliwa akisema ni vigumu kujua idadi ya watu waliouwawa, lakini kwa mujibu wa timu yake huko Saada kuna miili bado katika eneo la tukio, wengi wakiwa wamejeruhiwa.
Soma pia: Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen ziarani Hodeida
Shirika la msaraba mwekundu liliwahamisha baadhi ya majeruhi na kuwapeleka katika baadhi ya vituo ambavyo watapokea matibabu zaidi, lakini halikuweka wazi idadi ya watu waliouwawa katika shambulio hilo la gereza katika mji wa kaskazini mwa Saada.
Chanzo: AP