1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock amaliza ziara yake Irak kwa kutembelea Bundeswehr

10 Machi 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, amekamilisha ziara yake ya siku nne nchini Irak, kwa kutembelea ujumbe wa mafunzo wa jeshi la Ujerumani, Bundeswehr, katika mji mkuu wa Kurdistan wa Erbil.

https://p.dw.com/p/4OWoy
Annalena Baerbock im Irak
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock alikuwa mjini Erbil, kaskazini mwa Irak, ili kujua zaidi kuhusu ujumbe wa kijeshi wa Ujerumani ulioko nchini humo.

Katika kambi ya Stephan, mwanasiasa huyo kutoka chama cha watetezi wa mazhingira, alioneshwa gari la wagonjwa lenye uwezo wa kupita kila mahaka, ambalo linaweza kusafirishwa majeruhi.

Ameoneshwa pia silaha yenye uwezo wa kutatiza mashambulizi ya ndege zisizo na tubani za adui.

Soma pia: Baerbock akamilisha ziara ya siku nne Iraq

Kulingana na Wizara ya Ulinzi, takribani wanajeshi 300 wa Ujerumani kwa sasa wametumwa nchini Iraq na Jordan, na karibu 100 kati yao wako katika kambi ya kimataifa ya Erbil.

Bundeswehr imebadilisha kikosi chake cha mafunzo nchini Iraq ili kuwa cha ushauri zaidi. Hii inakusudiwa kuisaidia Iraq kuhakikisha usalama na kuendesha yenyewe mapambano dhidi ya wanamgambo wa kigaidi wa Dola la Kiislamu (IS).

Annalena Baerbock im Irak
Waziri Baerbock akionyeshwa picha za Wayazidi waliouwa katika makumbusho ya makaburi ya Kocho.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Makao ya ujumbe huo ni kambi ya Stephan iliyoko mjini Erbil, ambayo inaendeshwa na jeshi la Bundeswher.

Miaka michache iliyopita kundi la IS lilidhibiti maeneo makubwa nchini Irak na Syria, lakini tangu 2017, wapiganaji hao wa itikadi kali wanazingatiwa kuwa wameshindwa kijeshi, ingawa bado wanaedelea kufanya mashambulizi.

Wajibu wa jumuiya ya kimataifa

Siku ya Alhamisi waziri Baerbock alitembelea maeneo ulikofanywa ukatili wa kundi la IS mkoani Sinjar, kaskazini-magharibi mwa Iraq karibu na mpaka wa Syria.

Soma pia: Ujerumani kuwasaidia Wakurdi walioachwa bila makaazi

Akiwa katika kijiji cha Kocho ambako ulikofanyiwa baadhi ya ukatili mkubwa zaidi, Baerbock alisema jumuiya ya kimataifa, baada ya kushindwa kuzuwia mauaji ya halaki, inao wajibu kuhakikisha madhara yake hayahamishiwi kwa vizazi vijavyo, kwa kuwawajibisha waliotenda uhalifu huo.

Wafuasi hao wa itikadi kali waliuwa zaidi ya watu 5,000 wajamii ya Yazidi mwaka 2014, baada ya kuuteka mkoa huo. Maelfu ya watu waliuawa, kutekwa au kugeuzwa watumwa.

Annalena Baerbock im Irak
Waziri Baerbock akizungumza na mhusika wa kuondoa mabomu ya ardhini Ian Johnston kutoka shirika la Global Clearance Solutions katika mji wa Sinjar ulioharibiwa na IS.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Wayazidi wanaokadiriwa kufikia 210,000 waligeuka wakimbizi wa ndani, huku Ujerumani ikiwahifadhi watu wapatao 200,000 kutoka jamii hiyo.

Haizingatiwi kuwa salama kwa Wayazidi kurudi kwa jamii zao za nyumbani Iraq, hii ikiwa moja ya sababu kuu kwa nini watu wengi hawajarejea.

Umoja wa Mataifa na Bunge la Ujerumani zimelaani uhalifu wa wapiganaji hao na kuutaja kama mauaji ya halaiki.

Soma pia: Ujerumani kushirikiana zaidi na Iraq dhidi ya IS

Ujerumani imekuwa mwanachama muhimu wa muungano dhidi ya Dola la Kiislamu na ina uwepo wa nguvu katika mkoa wa Kurdistan.

Mwishoni mwa Oktoba, bunge la Ujerumani lilipiga kura kurefusha uwepo wa ujumbe wa Bundeswehr kwa mwaka mmoja, ili kuendeleza jukumu lake la ushauri dhidi ya kitisho cha IS.

Chanzo: dpa