1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yaikosoa Marekani kuhusu Asia Pasifiki

Josephat Charo
1 Oktoba 2024

Marekani imekosolewa na Korea Kaskazini kuhusu sera yake ya uchochezi kuelekea eneo la Asia Pasifiki.

https://p.dw.com/p/4lGVy
Balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa, Kim Song
Balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa, Kim SongPicha: Cia Pak/AP/picture alliance

Korea Kaskazini imeikosoa Marekani na washirika wake kwa kuchochea zaidi malumbano ya kijeshi kwa kushiriki mazoezi ya kijeshi katika eneo la Asia Pasifiki na kuendelea kuzungumzia kuhusu mabadiliko ya utawala katika taifa hilo lililotengwa kidiplomasia.

Balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa Kim Song amesema Korea Kaskazini inachukua hatua ambazo hakuzitaja, kujilinda yenyewe vyema zaidi.

Kim alikuwa akizungumza siku ya mwisho ya mkutano wa hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa jana Jumatatu, siku ambayo baadhi ya nchi zilizotengwa sana kidiplomasia zilihutubia pamoja na viongozi wa mataifa mbalimbali kama vile Canada na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Kim amesema Marekani haitendi haki kwa jumuiya ya mataifa na inautumia vibaya Umoja wa Mataifa kwa masilahi yake yenyewe. Hakuna kauli yoyote iliyotolewa na Marekani kujibu matamshi hayo ya Korea Kaskazini.