You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Sauti zetu
Vidio zetu
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Matangazo
Picha: DW
Picha: DW
Vidio zetu
Tazama vidio zetu hapa
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Fahamu zaidi kuhusu ugonjwa wa Parkinson
Parkinson ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa neva katika ubongo, na kusababisha harakati zisizodhibitika kama vile kutetemeka, kukakamaa kwa misuli, na ugumu wa kusawazisha mwili. Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa wa Parkinson umeongezeka mara mbili katika miaka 25 iliyopita, na kufikia zaidi ya milioni 8.5 duniani. #kurunziafya 11.11.2024
Wanawake wa Lebanon wakabiliwa na kitisho cha uzazi salama
Nchini Lebanon, idadi ya mimba kuharibika na watoto kuzaliwa mapema imekuwa ikiongezeka kwa sababu watu hulazimika kukimbia kila leo, kulinda usalama wao kutoana na mashambulizi ya Israel. DW imezungumza na mama huyu anayepigania uhai wa mwanae hospitalini.#kurunziwanawake
Harris kuchuana vikali na Trump. Nani kuibuka mshindi leo?
Kamala Harris na Donald kuchuana katika uchaguzi mgumu zaidi nchini Marekani
Upasuaji wa kubadilisha nyonga Tanzania
#Kurunzi Afya leo inakupeleka moja kwa moja hadi hospitali ya taifa ya Muhimbili Tanzania, kufahamu zaidi juu ya upasuaji wa kuwekewa NYONGA BANDIA. Upasuaji huu hufanyika kutokana na kusagika mifumo na matatizo mengine yanayochangia.
Mhamasishaji wa afya ya akili mitandaoni
Janeth ni msichana wa miaka 17 anayetumia mitandao ya kijamii kuwaelimisha vijana juu ya masuala ya afya ya akili na changamoto wanazokabiliana nazo. Japo vijana wengi hutumia mitandao, si wote ambao wanamuelewa. Lengo lake kuu ni kuona vijana wanatumia mitandao ili kuelimika na kufikia au kuzikamata nyadhifa mbalimbali.
Kilimo cha mwani kama kitega uchumi
Katika pwani ya Bahari Hindi, baadhi ya wanawake kutoka Tanzania wanaendeleza kilimo cha mwani kama kitega uchumi. Mwani, mmea wa baharini lakini wenye manufaa chungu nzima sasa umekuwa mbadala muhimu wa kilimo cha ardhini.
"Rumble in the Jungle": Miaka 50 ya Urathi wa Muhammad Ali
Tarehe 30 Oktoba 2024, tunaadhimisha miaka 50 tangu tukio la kihistoria "Rumble in the Jungle," ambapo Muhammad Ali alipambana na George Foreman huko Kinshasa. Tukio hili halikumpandisha tu hadhi Ali na kuwa nyota wa kimataifa lakini pia lilionyesha fahari ya watu wa Kongo. Jiunge nasi tunapochunguza urathi wa kudumu wa siku hiyo ya kihistoria kupitia ushuhuda wa kipekee na picha za kumbukumbu.
Ghana yashika nafasi ya kuongoza Jumuiya ya Madola
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola anaweza kushika nafasi hiyo kwa awamu mbili, za miaka minne.
Jasiri anaewapambania watoto Tanzania
Glorey Nisajile, ni msichana ambaye anawasaidia watoto watokao katika mazingira magumu na kuhakikisha kuwa wanapata mahitaji yao ya msingi, lakini lengo lake kubwa ni kuona watoto hawa wakijilinda kutokana na ukatili ambao mara nyingi hupitia. Anatamani kuona jamii ikiwasaidia watoto hawa na si kulisahau kundi hili.
Ushirikiano wa Ujerumani na Tanzania kuimarisha michezo
Vijana wa Kitanzania kutoka Mwanza, Zanzibar, Tanga na Moshi ni miongoni mwa wanufaika wa mafunzo yatakayotolewa na wakufunzi wa mchezo wa wavu kutoka Ujerumani. Ushirikiano wa nchi hizo mbili unakusudia kuimarisha sekta ya michezo haswa kwa chipukizi wa Tanzania.
Kongo: Wanawake Goma wajitosa kwenye bodaboda
Wanawake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameamua kuchukua jukumu la kufanya kazi ambazo zilikuwa zikihodhiwa na wanaume. Hatua hii inachochewa na ukweli kwamba wengi wamekuwa wakilea familia peke yao lakini pia changamoto za kiusalama katika eneo hilo. Sasa hawana wasi tena wenyewe wanasema mwendo mdundo fursa bila kujali jinsia.
Afya ya akili ni tatizo linalokuwa kwa wafanyakazi
Kundi la wafanyakazi linakabiliwa na changamoto kubwa ya afya ya akili, hii ni kutokana na changamoto kadhaa wanazokutana nazo. Kundi la waandishi wa habari ni miongoni mwa waathirika hao, lakini vipi wanakabiliana na changamoto hiyo?
Yvonne Aki Sawyerr ashinda Tuzo ya Ujerumani kwa Afrika
Meya wa mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, atunukiwa tuzo ya Ujerumani kwa Afrika. Yvonne Aki-Sawyerr ametuzwa kwa kujitolea kwake kwa wakaazi wa mji wake. Aliubadilisha mji wa Freretown kuwa bora kuishi kwa miaka sita pekee. Aliboresha huduma ya utupaji taka, usambazaji maji na anaendelea kuboresha hali ya mji huo hata zaidi. #DWKiswahili
Dansi ya zumba yatumika kama matibabu ya mwili na akili
Bila shaka unapocheza muziki unapata furaha hasa ukiwa unakwenda sawia na midundo, hata hivyo wataalamu wa tiba yamazoezi wanasema hayo ni mazoiezi mazuri ya kujenga mwili na misuri bila kusahau kuimarisha afya ya akili. Tumekuandalia video hii tazama dansi la zumba libayoboresha afya.
Mfahamu msichana mwalimu wa biashara
Salma ni msichana wa miaka 22 ambaye amekuwa akiwafundisha vijana namna ya kuanzisha biashara na kuziendeleza. Hata hivyo, si rahisi kwa baadhi yao kumuelewa lakini bado anamatumaini makubwa ya kufikia kundi kubwa la vijana, ili kuhakikisha kuwa wanajikwamua katika ajira na kuishi katika ndoto zao. #msichanajasiri.
Kurunzi: Kijana anayeuza miche ya maua
Jaffari Jokania mwenyeji wa Njiro Arusha kaskazini mwa Tanzania, amejiajiri katika biashara ya uuzaji wa miche ya maua, mboga za majani na miti, na biashara hii inamsaidia kuendesha familia yake. Mbali na sababu za kiuchumi, lakini pia kijana huyu anashauku ya utunzaji wa mazingira ili kukabilana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Jasiri wa programu za matumizi ya akili Mnemba
Sheila Fue ni msichana wa miaka 20 ambaye ni mwanatehama na muandaaji wa programu tofauti na matumzi ya akili mnemba. Mmwaka 2023 alishiriki mashindando ya tehama na kufika katika tano bora kimataifa. Sheila amechaguliwa kuwania tuzo 20 za Global Youth Award ambapo ni mtanzania pekee aliepata nafasi hii. #Kurunzi 27.09.2024
Kurunzi Afya: Tatizo la kukosa usingizi
Kukosa usingizi ni tatizo la kiafya ambalo linawakumba watu wengi, wataalamu wanaeleza baadhi ya sababu zinazochangia hali hiyo, ni kuota ndoto mbaya, msongo wa mawazo na matumizi ya pombe na dawa za kulevya. Zaidi msikilize daktari Msilikale Sengimana kutoka hospitali ya Njiro SAD Arusha.
Mfahamu Dinales, msichana anayetoa elimu ya Tehama
Kutokana na idadi ndogo na muamko wa wasichana kujifunza juu ya tehema imekuwa sababu ya Dinales kuwafundisha wasichana wengine juu ya umuhimu wa tehama na matumizi ya teknolojia japo si rahisi kwa jamii kumuelewa lakini matamanio yake makubwa nikuona idadi ya wasichana inaongezeka katika kada hii kadhalika na uelewa mkubwa katika matumizi ya teknolojia.
Ni vipi uvuvi na uchakataji dagaa unanawiri Kigoma?
Uchumi wa buluu husaidia kundi kubwa la wanawake kiuchumi. Nchini Tanzania, licha ya hofu ya mabadiliko ya tabia nchi na majanga yake, wanawake kutoka Kigoma wanapiga hatua kujijenga kiuchumi kutokana mazao ya baharini ikiwemo dagaa.
Msichana anayeelimisha jamii kuhusu ukatili dhidi ya watoto
Kutokana na ongezeko la vitendo vya ukatili, Dolice amemua kutoa elimu ya kujikinga na ukatili kwa watoto hasa shuleni.
Oumilkheir atutembelea baada ya miaka minne alipostaafu
Unamkumbuka Oumilkheir? Najua wafuatiliaji wetu wengi "wanaimiss" sauti yake adhimu enzi hizo akiwa nasi hapa Idhaa ya Kiswahili. Baada ya miaka kadhaa tangu alipostaafu, Bi Oumi, kama hapa tulivyopenda kumuita ametutembelea, na kupata fursa ya kuzungumza na mwenzetu John Juma.
Sumaiyya: Malkia wa barabara Zanzibar
Je, unaweza kubadili fani yako ulioipenda katikati mwa kilele kufuata fursa ya fedha na utofauti? Mtazame Sumaiyya alieipa kisogo taaluma ya habari na mawasiliano kwa ajili tu ya kufata fursa na utofauti.
Mwandishi kinda wa vitabu vya utalii Tanzania
Katika umri wa miaka 9, Queen Florence tayari ameandika vitabu 2 vya kuhamasisha utalii uliojificha nchini Tanzania. Mojawapo ya kitabu chake amekipachika jina la “NCHI YANGU TANZANIA”. Na huyu leo ndio msichana wetu jasiri.
Janga la homa ya nyani mkoa wa Kivu Kusini
Ruth Alonga ametembelea moja ya vituo vinavyowahudumia waathirika wa mpox huko Kivu Kusini kuona juhudi za kuudhibiti.
Mwanamke machinga mpambanaji
Night Ampurire ni mkaazi wa Entebbe Uganda. Ana mtoto mchanga ila hilo halimzuii kupambana ili kuhakikisha kwamba anachangia sehemu yake ya kipato nyumbani kwake. Matikiti maji ndiyo biashara yake licha ya gari lake kuukuu.
Fahamu zaidi kuhusu teknolojia ya upandikizaji mimba
Je unafahamu teknolojia ya #UpandikizajiMimba? Kwa wale wanaopata matatizo ya kupata mtoto kwa njia ya kawaida, upandikizaji mimba au IVF ni mojawapo ya njia wanazoweza kutumia. Fahamu zaidi kwenye KurunziAfya.
Ufafanuzi: Je ni nchi zipi zinahusishwa na vita vya Sudan?
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan kati ya jeshi la serikali na kundi la wanamgambo la RSF vimegharimu mamisha ya maelfu. Wapiganaji wa kimataifa na mamluki wamejiunga katika mapigano yasioonesha dalili ya kumalizika hivi karibuni.
Uungwaji mkono wa AfD mashariki mwa Ujerumani
Wakati ukuta wa Berlin ulipoanguka mwaka 1989, historia iliandikwa. Ulifungua mlango kwa Ujerumani kuungana tena. Lakini takriban miaka 35 tangu wakati huo, tofauti zingalipo kati ya Ujerumani magharibi na mashariki. Na hudhihirika kwenye chaguzi. Kwa miaka mingi Ujerumani Mashariki imekuwa ngome ya chama cha mrengo wa kulia AfD. Je uungwaji wao mkono watokana na nini?
Mfahamu mlimbwende wa Vyuo Vikuu Tanzania
Latricia ni msichana ambaye amelitwaa taji la ulimbwende kwa vyuo vikuu Tanzania 2024, ambapo safari yake ya kuanza kuzifuata ndoto zake ilianza akiwa na miaka 16, kutokana na taji lake anatarajia kuwa msemaji wa wasichana huku akitarajia kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ulimwenguni. #msichanajasiri @latricia_ian12
Kamala Harris: Uhusiano na Afrika
Utambulisho wa rangi wa mgombea urais wa Marekani Kamala Harris umerejea tena kwenye vichwa vya habari. Donald Trump, mpinzani wake, alizusha suala hilo kwa kudai Harris anawapotosha wapiga kura kuhusu hilo. Harris anajitambulisha kuwa Mweusi na kitu kingine zaidi ambacho ni cha uhakika ni —uhusiano wake na Afrika.
Msichana Jasiri : Mwelimishaji Afya ya Watoto
Kutana na Maria Mchome, msichana anayewaelimisha wazazi jinsi ya kilinda afya za watoto wao dhidi ya maradhi.
Miaka 25 ya Putin madarakani na ushawishi wa Urusi Afrika
Miaka 25 ya utawala wa Vladimir Putin nchini Urusi imeshuhudia kutanuka kwa ushawishi wake barani Afrika. Baada ya kipindi fulani cha kudumaa, mahusiano kati ya Afrika na Urusi yamebadili mwelekeo, na Moscow imejipatia nafasi kwenye mioyo ya waafrika wengi.
Mtetezi wa watoto wenye usonji
Msichana Jasiri: Lembe binti wa Kitanzania wa mfano wa kuigwa katika juhudi ya utetezi wa watoto wenye usonji.
Shambulizi la roketi lauwa watu 12 katika milima ya Golan
Shambulizi lililolenga katika uwanja wa michezo lauwa vijana 12 wakimwemo watoto wadogo wa hadi umri wa miaka 12.
Msichana jasiri aliyejitosa fani ya kuchomelea vyuma
Katika umri wa miaka 19, Sharifa Karim amekuwa msichana hodari na jasiri katika fani ya uchongaji na uchomeleaji vyuma. Anasema haikuwa rahisi wakati alipoanza kutokana na fani hii kuwa na idadi kubwa ya wanaume lakini anaona ufahari kuifanya kazi hii. #msichanajasiri
Monica Mkama Msichana Jasir Mjasiriamali
Monica ni msichana ambaye ameamua kujiajiri akiwa bado ni mwanafunzi, huku akiitumia biashara yake katika kuupiga kumbo umasikini. Kutokana na juhudi zake wapo ambao wamejifunza kutoka kwake. Je ni vipi aliweza kutoka kumiliki biashara moja hadi tatu?
Trump akubali kuwa mgombea wa Republican 2024
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amekubali rasmi uteuzi wa kuwania urais kwa tiketi ya Chama cha Republican katika mkutano mkuu uliotawaliwa zaidi na jaribio la mauaji dhidi yake.
Kurunzi Ujerumani: Tamasha la kulenga shabaha
Katika miji na vijiji vingi nchini Ujerumani, matamasha ya kulenga shabaha, maarufu kama “Schützenfest” hufanyika mara moja kwa mwaka.
Simba na Yanga zajiimarisha kuelekea msimu mpya wa soka
Kando na Clatous Chama, Yanga imewasijili Khomeini Abubakar na Boka Chadrak. Je, umeridhika na usajili wa klabu yako?
Unajua namna Yoga inavyoweza kukusaidia kiafya?
Nina uhakika unajua kitu kuhusu mazoezi ya Yoga, lakini unajua umuhimu wake kiafya? Kuna mengi unayoweza kujifunza ama kumshirikisha mwenzako kuhusu mazoezi haya. Tizama video hii kujifunza zaidi. #Kurunzi
Kituo cha elimu ya awali kwa watoto wakimbizi
Jamii za wakimbizi na wenyeji Kaskazini Magharibi mwa Uganda wameanzisha vituo vya kutoa elimu ya awali kwa watoto. Walimu na walezi ni wanajamii ambao wamejitolea kuendesha shughuli hiyo baada ya kupokea mafunzo maalum. Ebu tazama vidio na uwapongeze walimu hawa.
Dalili za tatizo la PCOS kwa wanawake
Wanawake wengi wenye ndevu ama nywele za usoni wanakabiliwa na matatizo ya kiafya ya PCOS yanayohusiana na homoni. Dalili nyingine za PCOS ni kuongezeka uzito, uso wenye mafuta na ugumu wa kubeba ujauzito. #kurunziafya #wanawake #pcos #afya
Neema Athuman: Muigizaji mdogo wa Tanzania
Neema Athuman: Muigizaji mdogo wa Tanzania
Monica Pereira ni DJ na mwalimu kutoka Cape Verde
Monica Pereira amevutia hisia za watu wa Cape Verde kwa kuwa maarufu kama DJ na mwalimu. Mapenzi yake ya muziki na hitaji la kupata pesa ndio sababu zilizomfanya aingie kwenye vilabu vya usiku, eneo ambalo bado linatawaliwa na wanaume nchini humo. Ebu tazama vidio na umpe neno mpambanaji huyu.
Fahamu maudhui yanayowavutia wasichana mitandaoni
Wasichana wamekuwa na matumizi mbalimbali ya mitandao ya kijamii lakini wengi wao hukumbana na changamoto nyingi, ambazo wengine huwaachia alama mbaya, ni kipi hasa wanatakiwa kujifunza kabla ya kuingia katika ulimwengu wa kidijitali ?
Fahamu namna ambavyo mionzi dawa inavyotengenezwa Tanzania
Cyclotron Kiube ni aina Mionzi dawa ambayo hutumika katika uchunguzi wa awali wa saratani kwa kupiga picha kwa kutumia PET-CT Scan ili kujua hatua ya saratani na kumsadia mtaalamu kujua ni aina gani ya dawa ambayo itakua na msaada kwa mgonjwa.
Germany inakabiliana vipi na uhalifu wa ukoloni Tanzania?
Ujerumani bado inaendeleza juhudi zake za kujivua gamba na yaliyotokea katika kipindi cha ukoloni nchini Tanganyika ambayo ni Tanzania bara ya sasa, mafuvu kadhaa ya binadamu walionyongwa yalisafirishwa kutoka nchini humo hadi Ujerumni kuhifadhiwa. Sasa familia za wahusika wameweka madai mezani. Sikiliza mahojiano.
Kituo cha kuwalea watoto bila malipo Nairobi
Huwa ni changamoto kubwa kwa mzazi aliye na mtoto mdogo kwenda kuchakarika kutafuta riziki. Lakini kuna mama mmoja Nairobi aliyeanzisha kituo kinachotoa suluhisho: kuwalea watoto saa za mchana bila malipo.
Matumizi yaliokithiri ya muguka na madhara yake kiafya
Matumizi mabaya ya muguka na dawa zingine za kulevya yamesababisha ongezeko kubwa la waraibu katika vituo vya kurekebishia tabia. Hata hivyo viongozi wa Mombasa kupiga marufuku usafirishwaji na uuzwaji wa aina hiyo ya bidhaa. Tazama video kuona madhara yake kiafya.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 1 wa 6
Ukurasa unaofuatia