1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Ugaidi

Wafungwa 900 watoroka katika uvunjaji gereza Congo Mashariki

20 Oktoba 2020

Wapiganaji wenye silaha wamewaachilia huru wafungwa wasiopungua 900 kutoka jela mjini Beni, mashariki mwa Congo, katika shambulio la kupanga mapema Jumanne, ambalo meya wa mji huo amelilaumu kwa waasi wa ADF.

https://p.dw.com/p/3kATD
Demokratische Republik Kongo l Soldaten in Beni - Epizentrum der derzeitigen Ebola-Epedemie
Picha: picture alliance/AP Photo/J. Delay

Zaidi ya wafungwa 900 wametoroka kutoka gereza la mji wa mashariki mwa Congo la BeniJumanne, amesema meya, wakiwemo wanachama cha kundi la waasi wa Kiislamu la ADF.

Modesta Bakwanamaha alisema waasi kutoka kundi la Allied Democratic Forces, ADF, na makundi mengine ya waasi walikuwa miongoni mwa waliotoroshwa gerezani na washambuliaji waliotumia vifaa vya kuchomelea.

Ni wafungwa 100 tu kati ya zaidi ya 1,000 walibakia kufuatia shambulio dhidi ya gereza kuu la Kangbayi na kambi ya kijeshi iliyolilinda gereza hilo, alisema Meya Bakwanamaha.

Karte DR Kongo, Beni
Ramani inayoonesha ulipo mji wa Beni,ambao umekuwa ukilengwa mara kwa mara na waasi wa ADF.Picha: DW

Soma pia: DRC bado yaendelea kupambana, mwaka mmoja baadae

"Kwa bahati mbaya, washambuliaji waliokuja katika idadi kubwa, walifanikiwa kuvunja mlango kwa kutumia kifaa cha umeme," Bakwanamaha aliliambia shirika habari la Reauters kwa njia ya simu. "Tunaamini ni ADF ndiyo walifanya uhalifu huu.

Kundi la Allied Democratic Froces, ADF, lenye chimbuko lake nchini Uganda, ambalo limejichimbia mashariki mwa Congo tangu miaka ya 1990, limeua zaidi ya raia 1,000 tangu mwanzoni mwa 2019, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, licha ya kampeni za mara kwa mara zinazolenga kulisambaratisha.

Kongo yaanzisha operesheni dhidi ya waasi

Polisi yatangaza idadi kubwa zaidi ya watoro

Wafungwa wawili walipigwa risasi na kuuawa wakati wa uvamizi, ambao ulianza majira ya saa kumi na nusu alfajiri kwa saa za Congo, ilisema polisi kwenye ukurasa wa Twitter. Polisi pia ilitoa idadi ya juu zaidi ya wafungwa - 1,300 - ikisema idadi kubwa walitoweka.  Idadi sawa ya wafungwa walitoroka wakati gereza hilo lilipovamiwa Juni 2017.

Soma pia: Raia 20 wauwa kaskazini-mashariki mwa DRC

Gereza la Kangbayi linawahifadhi wapiganaji mbalimbali wakiwemo wanachama wa vikosi vya ulinzi wa ndani na wapiganaji wa ADF. Bakwanamaha alisema kulikuwepo na uvumi kwamba wapiganaji wa ADF walikuwa wanapanga kuvunja gereza katika siku zilizotangulia shambulio hilo.

Uganda Gericht in Kampala | Rebellenführer Jamil Mukulu
Kiongozi wa kundi la ADF Alilabaki Jamil Mukulu,alikamatwa nchini Tanzania na kukabilidhiwa kwa mamlaka za Uganda ambako anakabiliwa na mashtaka ya uasi na ugaidi.Picha: AFP/I. Kasamani

Mwaka mmoja uliopita, jeshi lilianzisha kampeni kubwa ya kupambana na uasi wa ADF. Kufuatia kampeni hiyo, ADF ilitelekeza vituo vyake, na kujigawa katika makundi madogo madogo yanayohamahama, na kulipiza kisasi kwa raia.

Mashambulizi kadhaa yanayolaumiwa kwa ADF yamedaiwa pia na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, ingawa wataalamu wa Umoja wa Mataifa hawajapata ushahidi wowote wa mahusiano ya moja kwa moja kati ya makundi hayo mawili.

Vyanzo: RTRE, DPAE