1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Watoto milioni sita waathiriwa na Kimbunga Yagi

20 Septemba 2024

Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) linasema mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na Kimbunga Yagi yamewaathiri karibu watoto milioni sita katika eneo la kusini mashariki mwa Asia.

https://p.dw.com/p/4kubv
Myanmar Kimbunga Yagi
UNICEF inasema Kimbunga Yagi kimewaathiri watoto milioni sita wa kusini mashariki mwa Asia.Picha: Myanmar Fire Service Department/XinHua/picture alliance

Shirika la UNICEF limesisitiza kuwa watoto wanaendelea kutaabika kupata maji safi, elimu, huduma za afya, chakula na malazi.

Soma zaidi: Takbrini watu 300 wafariki kwa Kimbunga Yagi

Kimbunga Yagi kilisababisha upepo mkali na mvua kubwa kilipoyapiga karibu wiki mbili zilizopita mataifa ya Vietnam, Thailand, Laos na Myanmar huku idadi ya vifo ikiongezeka na kufikia watu zaidi ya 600 katika eneo hilo.

Mabadiliko ya hali ya hewa na ongezeko la joto litokanalo na shughuli za binadamu, vinachochea ongezeko la majanga ya asili.