You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Sauti zetu
Vidio zetu
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Mwangaza wa Ulaya: Nchi za EU zaanzisha ukaguzi wa mipakani
Umoja wa Ulaya unakabiliana na ongezeko la wahamiaji. Hilo limesababisha baadhi ya nchi wanachama wa umoja huo kuanzisha upya ukaguzi wa mipakani ndani ya eneo la nchi za Jumuiya hiyo maarufu Schengen, ambalo kwa kawaida hutakiwa kuruhusu usafiri bila ukaguzi wa watu na mali zao. Ungana na Bakari Ubena.
Je ni salama kujamiiana wakati wa ujauzito?
Je ni salama ama si salama kwa mama kufanya tendo la ndoa wakati wa ujauzito? Je mtoto aliye tumboni yuko salama kiasi gani? Je anaweza kudhurika kwa namna yoyote? Kuna ukweli gani kuhusu hili? Ungana nasi kwenye makala haya ya Afya Yako, tukizungumzia hili, sambamba na wataalamu.
Ruto atetea rikodi ya uongozi wake wa miaka miwili
Rais William Ruto wa Kenya ametetea rikodi yake ya miaka miwili madarakani akisema hakuna serikali ya nchi hiyo iliyowahi kuweka mikakati madhubuti ya kuiendeleza Kenya kuliko ile anayoiongoza. Rashid Chilumba alikaa na kiongozi aliekuwa ziarani mjini Berlin, Ujerumani na kujadiliana naye juu ya rekodi hiyo pamoja na mambo mengine.
Changamoto ya watoto wenye mahitaji maalumu Ghana
Watoto wenye matatizo ya mifumo ya fahamu wakati mwingine huonekana kama "wamelaaniwa" nchini Ghana na kutelekezwa.
Oumilkheir atutembelea baada ya miaka minne alipostaafu
Unamkumbuka Oumilkheir? Najua wafuatiliaji wetu wengi "wanaimiss" sauti yake adhimu enzi hizo akiwa nasi hapa Idhaa ya Kiswahili. Baada ya miaka kadhaa tangu alipostaafu, Bi Oumi, kama hapa tulivyopenda kumuita ametutembelea, na kupata fursa ya kuzungumza na mwenzetu John Juma.
Familia ya kada wa upinzani aliyeuawa Tanzania yateta
Hivi karibuni nchini Tanzania kumekuwa na matukio ya utekaji watu, kujeruhiwa na wakati mwingine kuuawa. Tukio la hivi karibuni linamhusu kada wa upinzani Ali Kibao aliyekutwa amefariki baada ya kutekwa kabla ya umauti. Sudi Mnette amezungumza na mtoto wake na mjane wake bi Amina Kibao kuhusu kifo cha mumewe katika makala ya Kinagaubaga.
Lishe bora katika kuandaa unyonyeshaji bora
Lishe bora ni kitu cha muhimu wakati mama anapokuwa mjamzito ili kujiandaa kwa ajili ya kumnyonyesha mwanae. Kama wengi tujuavyo, kila mama anahamasishwa kumnyonyesha mtoto wake miezisita ya mwanzo ili kupata lishe bora kabisa anayoihitaji katika ukuaji wake. Kuna mengi ambayo yatakunufaisha ukisikiliza makala ya Afya yako.
Mwangaza wa Ulaya:Viongozi wa EU wajadili msaada kwa Ukraine
Mzozo kati ya Urusi na Ukraine ambao unaelekea kuingia katika mwaka wa tatu unazidi kutokota. Mwishoni mwa mwezi Agosti, mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya walijadiliana kuhusu kuongeza msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Lakini pia mzozo huo umezusha hali ya hofu kwa mataifa ya Baltic yanayopakana na Urusi ambayo yanahofia kwamba wakati wowote wanaweza pia kushambuliwa. Ungana na Bakari Ubena.
Kukatika kwa mawasiliano baina ya marafiki, tatizo ni nini?
Hali ya kupotezeana imekuwa jambo la kawaida hasa baada ya marafiki kuunganishwa kupitia mitandao ya kijamii.
Wanawake na Maendeleo
Bi. Asawar Mustafa, mwanamke mkimbizi kutoka Sudan anayefanya kazi ya ufundi wa magari nchini Libya amefanikiwa kwa vitendo na kuonesha kwamba mwanamke pia anaweza kuwa fundi gereji hodari na kwamba kazi hiyo si ya wanaume pekee. Makala hii imeandaliwa na Zainab Aziz.
Dhulma dhidi ya waandishi habari Kenya
Katika makala ya Mbiu ya Mnyonge leo, mwandishi wa DW Musa Naviye anaangazia dhulma walizopitia waandishi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali nchini Kenya. Baadhi ya waandishi walipigwa risasi na kupitia madhila mengine mikononi mwa maafisa wa polisi wakati walipokuwa wakifanya kazi yao ya kuuhabarisha umma.
Sura ya Ujerumani: Umaarufu wa AfD Ujerumani Mashariki
Makala ya Sura ya Ujerumani inamulika je, ushawishi mkubwa wa chama cha AfD mashariki mwa Ujerumani unatokana na nini?
Kutoka London hadi Lagos peke yake kwa gari
Fikiria, alilala na kula wapi? Vipi kuhusu usalama wake? Kutana na msichana Pelumi mzaliwa wa Lagos, Nigeria aliyekulia London Uingereza. Alitaka kuvunja rekodi ya ulimwengu kwa kuwa mwanamke wa kwanza aliyesafiri mwenyewe kati ya mabara mawili ya Ulaya na Afrika. Tizama safari yake ya kutoka London hadi Lagos akiendesha mwenyewe gari dogo. #Vijanamubashara
Je, Polisi wapewe mafunzo maalumu kukabili maandamano?
Wakati wa maandamano maafisa polisi hushuhudiwa wakitumia nguvu kupita kiasi. Katika vidio hii Mtaalamu wa usalama wa Kenya Byron Adera anachambua jinsi polisi wanapaswa kuyadhibiti maandamano. #vijanamubashara
Mji wangu - Soweto
Kitongoji cha Soweto kinapatikana viungani mwa jiji la Johannesburg. Kimekuwa jukwaa la baadhi ya matukio muhimu katika historia ya Afrika Kusini. Mmoja wa wasanii maarufu wa mitaani mjini humo, Senzo Nhlapo, anatutembeza katika kitongoji hiki chenye uchangamfu.
Wanawake na Maendeleo: Jeniffer Shigoli mtetezi wa haki za wanawake na mabinti
Jeniffer Richard Shigoli ni mwanaharakati anaesimamia masuala ya usawa wa kijinsia kupitia kampeni yake ya 'Binti Huru' anawasaidia watoto wa kike walio shuleni waweze kuepukana na vikwazo vitokanavyo na hedhi sabamba na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake walio katika mazingira duni ili waweze kuepukana na umasikini.
Je unasoma masharti wakati wa manunuzi mtandaoni
Sema Uvume je umeshakutana na masharti na makubaliano ama kwa kimobo Terms and Agreements wakati unaponunua vitu mitandaoni? Je, unayasoma na kuyaelewa masharti hayo? Athari za kutoyasoma ni zipi? Sema Uvume inakupa majibu mtayarishaji ni Suleman Mwiru.
Ipi sababu ya kijana kusoma vitabu vya hadithi kuliko dini?
Katika kipindi cha Vijana Mubashara, Jacob Safari anauliza je unafikiri ni kwanini vijana wako radhi kusoma vitabu vya hadithi au riwaya kuliko vitabu vya kidini?
Msimamo wa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar
Ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi kufanyika mwakani, mwandishi wetu wa Zanzibar Salma Said, amezungumza na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, kujua je juhudi gani ambazo wamezifanya kuinusuru serikali ya umoja wa kitaifa kabla kuporomoka?
Vijana Mchaka Mchaka - Shauku ya kupokea mshahara wa kwanza
Makala ya Vijana Mchaka Mchaka inamulika shauku ya vijana ya kupokea mshahara wa kwanza na umuhimu wa kuuwekea malengo.
Tatizo la watoto kukosa umakini au nguvu kupita kiasi-ADHD
Kurunzi afya leo inamulika tatizo la afya la kukosa umakini au nguvu kupita kiasi, kitaalamu likijulikana kama ADHD miongoni mwa watoto. Baadhi ya Watoto hukumbwa na tatizo hilo kuanzia umri mdogo huku wazazi wasijue kuwa ni tatizo la kiafya, ambalo kulingana na WHO liko miongoni mwa matatizo ya afya ya akili. Fathiya Omar amezungumza na wataalam mjini Mombasa. #Kurunziafya
Changamoto za uzazi wa mpango nchini Sudan Kusini
Makala ya afya yako inatizama changamoto za upangaji uzazi kwa kundi kubwa la wanawake na wasichana wa Sudan Kusini.
Ukatili wa kingono katika vita vya Sudan
Mbiu ya Mnyonge hivi leo inalia na wanawake wa Sudan wanaoandamwa na ukatili wa kingono katikati mwa balaa la vita.
Maandamano ya vurugu Uingereza
Uingereza inakabiliwa na maandamano ya vurugu kufuatia mauaji ya wasichana watatu mnamo Julai 29 huko Southport. Washiwishi wa mitandaoni wenye mafungamano na itikadi za siasa kali za mrengo wa kulia walizagaza uvumi kuhusu mhusika wa mauaji hayo na kusema ni muislamu mwenye itikadi kali aliyewasili Uingereza hivi karibuni, na hivyo kuchochea chuki dhidi ya wahamiaji na waislamu nchini humo.
Unaweza kuwa na mahusiano na mpenzi aliebuniwa kwa AI?
Kama ungepata nafasi ya kumtengeneza mwenyewe mwenzi wako kwa namna unayotaka mwenyewe, ungependa awe vipi? Ni swali analojuliza mtafiti wa masuala ya kujamiiana Kaamna Bhojwani.
Mpenzi aliyetengenezwa kwa teknolojia ya Akili Mnemba
Kama ungepata nafasi ya kumtengeneza mwenyewe mwenzi wako kwa namna unayotaka mwenyewe, ungependa awe vipi? Teknolojia ya Akili Mnemba sasa inatumiwa kutengeneza mpenzi mwenye sifa na hulka anayoitaka mtu. Fuatilia hapa katika makala ya Sema Uvume.
Tuzo za fasihi na waandishi wanawake wa Kiafrika
Tuzo ya Fasihi ya Safal-Cornell inakaribia kutimiza miaka 10 tangu ilipoasisiwa mwaka 2014 na washindi wake wa kwanza kutangazwa mwaka 2015. Tuzo hiyo imevutia ushiriki wa maelfu ya wanafasihi kwenye mataifa yanayozungumza Kiswahili. Mohammed Khelef anazungumza na Anna Samuel, mshindi wa kwanza aliyeizindua tuzo hiyo ya riwaya yake ya Penzi la Damu, juu ya safari ya mwandishi wa fasihi.
Sudan: Je makubaliano ya kuvimaliza vita yanaweza kufikiwa?
Zainab Aziz amewakaribisha wachambuzi kuijadili hali ya Sudan ambako majenerali wawili wanapigana kuidhibiti nchi hiyo.
Fahamu kuhusu wizi wa taarifa binafsi mtandaoni
Wizi wa taarifa binafsi ni uhalifu wa mtandaoni ulioshamiri nyakati hizi dunia ikishuhudia maendeleo makubwa ya teknolojia. Sambamba na tatizo hilo, makala ya Sema uvume leo inaangazia pia wimbi kubwa la ujumbe mfupi unaolenga kuwahadaa na kuwaibia watu. Sikiliza hapa kufahamu zaidi
Belarus: Miaka 30 ya utawala wa Lukashenko
Katika siasa za ulaya kwa miongo kadhaa, tumeshuhudia viongozi wa mataifa mbalimbali wakipishana madarakani. Lakini Alexander Lukashenko amekuwa rais wa Belarus kwa miaka 30. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 69, ameitawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma na kuwa na udhibiti kamili. Kipi kimemuwezesha kusalia madarakani kwa muda wote huo? Ni mbinu gani anazozitumia ili kutoyumbishwa?
Habineza: Nilijitabiria kupata angalau asilimia 55 ya kura
Aliyekuwa mgombea wa uchaguzi wa rais uliomalizika nchini Rwanda Frank Habineza aliyeibuka nafasi ya pili kwa kupata asilimia 0.5 amezungumza na Rashid Chilumba katika Kinagaubaga. Ameeleza kuwa alikuwa na matarajio ya kupata asilimia nyingi katika uchaguzi huo.
Scholz ashiriki maadhimisho ya miaka 80 ya kumpinga Hitler
Kansela Olaf Scholz amesema demokrasia ya Ujerumani inategemea juhudi za kila mmoja bila kuchoka.
Kinagaubaga: Tume ya uchaguzi nchini Tanzania ni huru?
George Njogopa anazungumza na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania, Ramadhan Kailima kuhusu uboreshaji daftari la wapigakura, malalamiko ya upinzani kutoshirikishwa kwenye michakato ya tume na ikiwa ni kweli tume hiyo ya kusimamia uchaguzi ni huru.
Vyakula maarufu vya mitaa ya Kinshasa
Pouleti Mayo, Ntaba na Ngulu ya Kapela ni vyakula maarufu vya mitaa ya jiji la Kinshasa. Vinapatikana kila kona na kwa haraka. Je, hapo mtaani kwako chakula gani ni maarufu hata usiku wa manane kinapatikana?#77asilimia #vijanamubashara
Jukwaa la Manufaa
Angela Mdungu anakupa nafasi ya kutoa dukuduku pongezi, maoni au ushauri kuhusu masuala yanayohusu jamii inayokuzunguka.
Wakenya wageukia dawa za kiasili na kuacha za hospitalini
Wimbi la madadiliko linazidi kupepea nchini Kenya, na kila linapopita linaleta athari chanya, likibadilisha mawazo ya wakenya wengi wanaokumbatia dawa za kiasili na kuachana na dawa za hospitalini. Shisia Wasilwa anakufahamisha ni kwanini hilo linashuhudiwa nchini humo.
Uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi Ujerumani
Uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi Ujerumani unavyokwamisha shughuli mjini Mittweida
Mitandao ya kijamii inaweza kuleta mageuzi ya siasa Afrika?
Makala ya Vijana Mchaka Mchaka inamulika nafasi mitandao ya kijamii barani Afrika katika mageuzi ya kisiasa.
Msigwa: Chadema imepoteza mwelekeo wake wa kisera
Kambi ya upinzani nchini Tanzania imepata pigo kubwa baada ya mwasiasa mkongwe wa upanzani mMchungaji Peter Msigwa kutimkia chama tawala CCM huku akitangaza chama chake cha zamani kukosa mwelekeo katika masuala kadhaa ikiwemo demokrasia na mwelekeo wa kisera, lakini anakoselewa kuwa ni mwanasiasa mwenye uchu wa madaraka. Msikilize akijibu tuhuma hizi
Vikosi vya Tanzania vitaendelea kubaki Msumbiji
Katika wasaa huu wa takriban dakika kumi Sudi Mnete anazungumza na waziri wa Ulinzi nchini Tanzania Stergomena Tax kutaka kujua mwenendo wa oparesheni ya kijeshi ya vikosi vya Tanzania nchini Msumbiji.
Waasi wa M23 wakanusha kushirikiana na jeshi la Rwanda
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 wameweka chini mtutu wa bunduki ili kupisha misaada ya kiutu kuingia katika maeneo yanayoshuhudia mapigano makali. Hatua hii inafanyika katika wakati ambapo Rwanda inashutumiwa kupeleka vikosi vyake kupigana mashariki mwa Kongo, je Kigali inaunga mkonoM23?. Katika Kinagaubaga sikilize msemaji wa M23
Akili mnemba itapunguza vijana kutumia maktaba?
Ukweli usiopingika ni kwamba akili mnemba ama akili ya kubuni inatumiwa na wengi katika masuala mbalimbali kwenye sekta ya elimu. Wanafunzi pia wanatumia teknolojia hii, lakini wasiwasi wa baadhi ya wafuatiliaji ni kwamba teknolojia hii inaweza kusababisha vijana wengi kutotumia vitabu na hata maktaba kwa ajili ya kujisome. Sikiliza mjadala wa vijana.
Vijana wanapata wenza kupitia mitandao ya mahusiano
Mitandao ya kijamii pamoja na mitandao ya kimahusiano ama Dating Apps zinatumiwa na vijana katika kupata wenza wa maisha, lakini wapo baadhi ya watu wanaona hiyo sio njia sahihi ya kumtafuta mwenza wa kuanzisha nae familia ilio bora, kwa hoja kwamba wanaweza kutofautiana kitamaduni na hata kiimani ambao ni msingi wa maisha.
Ufaransa: Matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa Bunge
Matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa Bunge nchini Ufaransa, yaliwashangaza wengi baada ya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally kujikuta katika nafasi ya tatu wakati ambapo katika duru ya kwanza kilikuwa kikiongoza. Siasa za Ufaransa zimejikuta katika hali ya mkwamo, kwa kuwa hakuna muungano wowote uliopata kura za kutosha ili kuwa na udhibiti kamili wa Bunge.
08.07.2024: Matangazo ya asubuhi
Sikiliza matangazo ya asubuhi ya DW Kiswahili
Umasikini unavyowatesa wastaafu Germany
Mstaafu mmoja kati ya watano nchini Ujerumani anakabiliwa kuwa katika hatari ya umasikini, kulingana na ofisi ya takwimu ya Ujerumani. Idadi ni kubwa zaidi hasa kwa upande wa wanawake
Mamlaka za afya Uganda zatahadharisha juu ya homa ya nyani
Ugonjwa wa homa ya nyani una madhara makubwa kwa akina mama wajawazito na huenda ukasababisha kuharibika mimba.
Unajua namna Yoga inavyoweza kukusaidia kiafya?
Nina uhakika unajua kitu kuhusu mazoezi ya Yoga, lakini unajua umuhimu wake kiafya? Kuna mengi unayoweza kujifunza ama kumshirikisha mwenzako kuhusu mazoezi haya. Tizama video hii kujifunza zaidi. #Kurunzi
Akili mnemba katika soka
Makala ya Sema Uvume leo inamulika namna akili mnemba inavyotumika na inavyotarajiwa kutumika katika maeneo mbalimbali ya mpira wa miguu.
Mabadiliko ya uongozi kwenye Jumuiya ya kijeshi ya NATO
Kwa mujibu wa taarifa, Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte, anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa jumuiya ya kujihami ya NATO baada ya mpinzani wake rais wa Romania Klaus lohannis, kujoindoa kwenye kinyangànyiro. Mtayarishaji Zainab Aziz
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 1 wa 4
Ukurasa unaofuatia